Monday , 21st Nov , 2016

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, imesema kuwa kufikia mwaka 2030 inatarajia kupunguza moja ya tatu ya vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Dkt. Magreth Mhando

Akifungua mkutano wa madaktari wakuu kutoka mikoa mbalimbali nchini, uliofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Tiba  kutoka wizara hiyo Dkt. MAGRETH MHANDO amesema hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Afya NIMR

Utafiti huo umebainisha kuwa magonjwa yasiyo ambukiza nchini Tanzania unaonesha kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanaongezeka kwa kasi duniani ikiwemo Tanzania.

Dkt. MHANDO amesema, magonjwa hayo yameongezeka kutokana na idadi ya watu wanaovuta sigara kufikia asilimia 15.9, wanaokunywa pombe asilimia 29.3, wenye uzito uliopita kiasi asilimia 34.7, shinikizo la damu asilimia 25.9 na wagojwa wa kisukari asilimia 9.1.

Dkt. MHANDO amesema kuwa Wizara ya Afya, imejipanga kupambana na magonjwa hayo, kwa kuboresha huduma za kinga na tiba ya utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe, pia kufikia mwaka 2020 kupunguza nusu ya Idadi ya vifo duniani na ajali za barabarani.