Waziri Mkuu atoboa siri kupungua mizigo bandarini
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kupungua kwa mizigo bandarini hakusababishwi na sera ya serikali ya awamu ya tano, bali ni suala la kidunia linalosababishwa na kushuka kwa sekta ya usafirishaji wa mizigo duniani kote, na siyo Tanzania pekee.