Waathirika mafuriko Kilosa wahitaji msaada
Zaidi ya hekari 1,000 za mazao ya chakula zimesombwa na maji, nyumba 10 zikianguka na nyingine zaidi ya 100 zimezingirwa maji katika kijiji cha Changalawe Kata ya Masanze wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua.