Azam yazifuata Yanga na Simba kombe la shirikisho.
Klabu ya soka ya Azam imekamilisha idadi ya timu nane za kucheza Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wenyeji, Panone FC jioni ya leo uwanja wa Ushirika mjini Moshi, Kilimanjaro.