Wakuu chuo cha utumishi wa umma wasimamishwa kazi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki amemsimamisha kazi Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Bw. Said Nassor pamoja na wakuu wengine wawili wa matawi ya chuo hicho.