Aliyefia vitani Ukraine kuzikwa Mbeya
Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo aliyefariki dunia akipigana vita nchini Ukraine upande wa Urusi utaagwa hii leo jijini Dar es Salaam, na utasafirishwa kupelekwa Kijiji cha Kasyeto Tukuyu mkoani Mbeya, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Januari 28, 2023.