"Hakuna ajali ya ndege iliyoua na kujeruhi"- DC
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, amesema kwamba kiuhalisia hakuna ajali ya ndege ya abiria iliyotokea wilayani humo na kwamba kilichofanyika leo ni zoezi la utayari wa kukabiliana na ajali za aina hiyo lililoandaliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.

