Polisi wazungumza ajali iliyoua watano
Watu watano wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster kugongana na gari la mizigo aina ya Mitsubishi Canter, katika eneo la Mwavi, Kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.