TPLB yamfungia Gadiel Michael michezo mitatu
Mchezaji Simba SC, Gadiel Michael amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) na TPLB kwa kosa la kulazimisha kuingia uwanjani saa 4:25 asubuhi ya siku ya mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City kwa kile alichoeleza alitaka kukagua kiwanja.