Wanafunzi watumia miti chooni Tabora
Wanafunzi wa shule ya msingi Tulieni iliyo katika kijiji cha Tulieni kata ya Ndono wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamekuwa wakilazimika kutumia karatasi ngumu na miti kujisafisha chooni kutokana na kukosekana kwa maji hivyo kuiomba serikali kuharakisha maboresho ya miundombinu shuleni hapo.