Kiluvya, Mbao Fc,CDA kucheza Ligi Daraja la kwanza
Timu za Kiluvya United ya Pwani, Mbao FC ya jijini Mwanza, Mji Njombe kutoka mkoa mpya wa Njombe na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma zimepanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuongoza katika misimamo ya makundi yao ya Ligi Daraja la Pili (SDL).