Wizara yalaumiwa kwa kuchukua ardhi kabla ya fidia
Baadhi ya wabunge katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameitupia lawama Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kitendo chake cha kuamua kuwanyang'anya ardhi wananchi kabla ya miradi husika haijakamilika.