Wizara yakemea upotoshaji kuhusu homa ya Dengue
Wizara ya Afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania imewataka wananchi watambue kuwa ugonjwa wa dengue upo na wapuuze taarifa za upotoshaji unaofanywa kupitia mitandao ya kijamii, simu za mikononi na mikusanyiko ya watu kuwa ugonjwa huo haupo.