Mahakama yatupilia mbali ombi la Ponda
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya kufanya marejeo ya kuondoa shitaka la kukaidi amri halali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda.