RC Sendiga aagiza TAKUKURU kuchunguza miradi
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa haraka juu ya miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na hospitali katika Manispaa ya Sumbawanga ili kuona endapo kuna matumizi mabaya ya fedha za umma.