Ajali yaua mmoja Morogoro na kujeruhi 33
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Alfonce, amefariki dunia na wengine 33 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu kugongana kwa nyuma baada ya gari lililokuwa limetangulia mbele kusimama ghafla katika eneo la Makunganya nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.