Polisi wawataka wananchi kutoa ushirikiano
Jeshi la Polisi Wilaya ya Geita limelalamikia juu ya wananchi wanaotakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi na Mahakamani juu ya kesi za Ukatili kushindwa kutoa ushahidi hivyo kesi nyingi zimekuwa zikimalizwa nyumbani na kupelekea watuhumiwa wa vitendo hivyo kushindwa kupata adhabu.