Monday , 10th Oct , 2022

Jeshi la Polisi Wilaya ya Geita limelalamikia juu ya wananchi wanaotakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi na Mahakamani juu ya kesi za Ukatili kushindwa kutoa ushahidi hivyo kesi nyingi zimekuwa zikimalizwa nyumbani na kupelekea watuhumiwa wa vitendo hivyo  kushindwa kupata adhabu.

Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto wilaya ya Geita Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Christina Katana

Malalamiko hayo yametolewa na Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto wilaya ya Geita Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Christina Katana wakati wanatoa Semia kwa wasanii ili waweze kutengeneza maudhui yatakayoifundisha jamii kuacha ukatili iliyoandaliwa na shirika la Plan International, anasema matukio ya ukatili yanazidi kuongezeka kwa wanawake na watoto kike huku mashahidi wamekuwa wakikwamisha hatua za hukumu kutokana na kutotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

"Wanaripoti lakini kuripoti huko bado kunaonekana kwamba ni kama chanzo cha kufanya Ile kubargain kwamba wanataka kukubaliana, kuyasuluhisha kuyamaliza kwahiyo ili mtu aongeze Ile nguvu ya yeye kupata anachokipata anaona akiongeza Jeshi la Polisi katikati kwamba nimetoa taarifa Polisi itachukuliwa hatua anaona kama ni hatua ambayo itamsaidia yeye  kupata kile anachokihitaji kwahiyo watu kutoa taarifa na kupotea ipo na ndio maana wakati mwingine, matukio ya Ukatili sisi wenyewe kama Jeshi la Polisi tunasimama kama walalamikaji ili kesi iweze kwenda mbele, mtu anakuja anatoa taarifa za Ukatili lakini hataki ajukikane, hataki aonekane tunaivaa sisi kama sisi kwa sababu sisi ni wataalam wa kusimamia hilo lakini tunakuta vitu vingine vinapelekea haki inapatikana", alisema Katana.

Kwa  upande wake Msimaizi wa masuala ya jinsia kwenye mradi wa KAGIS Hildegada Mashauri  anasema wameamua kutumia wasanii kuelimisha jamii kwa sababu wao wanawafikia watu wengi kupitia kazi zao.
"Tuna Imani tutatoka na mpango kazi ambao hao hawa wasanii sasa katika kazi zao wataenda kufikisha ujumbe na kuelezea jamii nzima juu ya changamoto zote ambazo tumekuwa tukiziona, tunazisikia wasichana wanazipitia na tukiwa tunajua pia wao kama wasanii wana  jukumu vilevile la kuhakikisha kwamba wanaibadilisha jamii mitazamo yao juu ya msichana juu ya maswala mazima ya ukatili wa kijinsia", alisema Mashauri.

Baadhi ya wasanii wanasema jinsi watakavyotumia Sanaa zao kuelimisha jamii kuacha Ukatili wa kijinsia.

"Tumeona jamii nyingi Sana zikiendelea na zoezi la Ukatili yani vitendo vya ukatili, kwahiyo sisi kama wasanii tutahakikisha kwamba tutaibadilisha jamii kwa kuweza kuielimisha kwa kuweza kuionya kuacha tabia hizi ambazo zimeendelea ambazo zinaoelekea taifa letu kuwa na kukosa nguvu kazi kwenye Taifa", alisema Paulo