Rais Museveni awaomba msamaha Wakenya
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amewaomba msamaha Wakenya kufuatia mtafaruko uliosababishwa na mtoto wake, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika ujumbe wa kwamba yeye na jeshi lake wanaweza kuliteka Jiji la Nairobi kwa wiki mbili tu.