Akamatwa kwa kutapeli milioni 150 za magari
Polisi mkoa wa Iringa, wanamshikilia Michael Mbata, mkurugenzi wa kampuni ya Foa Motors kwa tuhuma za makosa ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha milioni 150, kutoka kwa wakazi wawili mkoani humo kwa ahadi ya kuwaagizia magari aina ya Howo kutoka Japan na kisha kuzima simu.