Shaka ataka wasomi wasio na ajira watambuliwe
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka, ametoa mwelekeo wa kutatua changamoto ya ajira kwa vijana nchini hasa wasomi wa vyuo vikuu huku akitaka wasomi hao watambuliwe na kisha wawezeshwe na hatimaye kujiajiri.