Mapendekezo ya sheria mpya ya usimamizi wa maafa
Serikali imeandaa mapendekezo ya kutungwa kwa sheria mpya ya usimamizi wa maafa ili kuweka mfumo wa udhibiti na uratibu wa maafa kwa ajili ya hatua za kuzuia na kupunguza madhara ya majanga, kujiandaa kukabili na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea.

