
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyokutana katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma kujadili muswada wa sheria ya usimamizi wa maafa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene, amesema kutungwa kwa sheria hiyo ni kuifuta sheria iliyopo sasa ya mwaka 2015 sura ya 242.
Mhe. Simbachawene ameeleza kwamba awali masuala ya maafa hayakuwa na mfumo wa kisheria wa uratibu hali ambayo imekuwa ikisababisha mgongano wa majukumu hivyo kutungwa kwa sheria hiyo kutaainisha madaraka, wajibu, maamuzi, utunzaji wa rasilimali na muono unaozingatia taarifa za hali ya hewa.