Usambazaji wa maji kutoka Ziwa Tanganyika
Wizara ya Maji imeanza kuangalia uwezekano wa kuanzisha mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Tanganyika ili kuyasambaza katika miji mikubwa ya mikoa ya Rukwa, Katavi na kuyaunganisha maji hayo na maji yanayotoka Ziwa Victoria katika mkoa wa Tabora.