
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema hayo mara baada ya kushirikiana na wataalamu wa Wizara hiyo kutembelea na kukagua baadhi ya maeneo yanayoweza kuwa vyanzo vya maji katika miji ya Karema, Kabwe na Kasanga mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usambazaji maji kutoka Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Juma Waziri amesema baada ya kukagua maeneo hayo wamebaini kuwa upo uwezekano wa maji ya Ziwa Tanganyika kusambazwa kwa wananchi ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa huduma ya maji.