Mawakili wa Zumaridi waeleza alivyokosa imani
Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi namba 10 inayomkabili Mfalme Zumaridi na wafuasi wake nane wameonesha kutokuwa na imani na Hakimu anayeendesha kesi hiyo na kuiomba Mahakama kutolea maamuzi ya sababu walizowakilisha ili ushahidi uendelee kutolewa.