Bidhaa za misitu lazima zipigwe chapa - Waziri
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, amewataka watengenezaji wote wa bidhaa za misitu nchini wahakikishe kuwa wanaweka alama inayoonesha bidhaa zao zimetengenezwa Tanzania yaani "Made in Tanzania" ili bidhaa hizo zijulikane kuwa zimetengenezwa Tanzania.