"Kuhusu Loliondo taarifa ni ya Waziri Mkuu - Tulia
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, amesema kwamba taarifa iliyonayo Bunge kuhusu Loliondo na Ngorongoro ni ile ya serikali iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kwamba Bunge haliwezi kutumika kujibu maneno ya mitandaoni.