Mchina wa miaka 42 anatafutwa kwa mauaji
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mtuhumiwa Zheng Lingyao (42), raia wa China na mkazi wa jiji hilo kwa tuhuma za kumuua Fu Nannan (26) raia wa China mfanyabiashara na mkazi wa Kalenga Ilala, uchunguzi umebaini kulikuwa na tatizo la masuala ya mapenzi.