Aweso awataka wakandarasi kuacha visingizio
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amewataka wakandarasi wanaojenga bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kata ya Masaka mkoani Iringa, kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati uiliopangwa, ili kusaidia wananchi kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.
