Coca Cola Kwanza yawaleta karibu wadau na wateja

Ijumaa , 24th Mei , 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza Basil Gadzios, amesema kampuni hiyo itaendelea kukutana na kuwa karibu na wateja wake kupitia hafla mbalimbali wanazoziandaa.

Wadau mbalimbali wakipata chakula cha jioni (Futari) kilichoandaliwa na Coca Cola Kwanza.

Hayo ameyasema leo Mei 24, 2019, kwenye hafla ya chakula cha jioni wakati huu wa mfungo wa Ramadhani (Futari), iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

''Tumejumuika hapa kwenye chakula cha jioni ikiwa ni sehemu tu ya kampuni yetu kuwakumbuka wateja wetu wakati huu wa mfungo na huu ni mwanzo tu, tutaendelea kufanya hivi kwa makundi yote'', - amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Coca Cola Kwanza, Haji Mzee Ally, amesema wamejisikia vizuri kupata baraka za Ramadhani kwa kuandaa futari hiyo kwaajili ya waislam na wadau wao kwa ujumla.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau kutoka vyombo tofauti vya habari, pamoja na wateja mbalimbali wa vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni hiyo.