Jumatatu , 27th Mar , 2023

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo WAMA Mama Salma Kikwete amewataka makampuni mengine kuiga mfano wa Kampuni ya Coca cola kwanza ambayo imefanya kwa wajasiriamali zaidi ya 300 kuwapa vifaa vya kuinua biashara zao ikiwemo mitungi ya gesi.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete na Mdau wa Maendeleo ya Wanawake ametoa rai hizo kwenye hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Cocacola Kwanza kwa ajili ya kuwakabidhi wanawake wajasiriamali Majiko na mitungi ya gesi 100 ikiwa ni ajenda ya kampuni hiyo kuwajengea uwezo wa kiuchumi wajasiriamali nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza Bw. Unguu Sulay akizungumza kwenye hafla hiyo alisema ajenda hiyo imeungwa mkono na wadau mbalimbali ikiwemo kampuni ya ORXY Gases ambayo imetoa majiko waliyokabidhiwa akina mama hao pamoja Taasisi ya Ustawi wa Jamii ambayo imetoa elimu kwa wajasiriamali hao kujitambua na kuepuka msongo wa mawazo, kutunza vitabu vya kumbukumbu ya mahesabu na huduma kwa wateja.

Hafla hiyo ilianza kwa wajasiriamali hao kuhudhuria darasa la mafunzo ambapo baadhi yao wakaeleza manufaa waliyopata