Jumatatu , 3rd Oct , 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB, Dkt. Redempta Mbatia (kushoto) katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kauli mbiu "Sherehekea Huduma"

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akikabidhi zawadi kwa mmoja ya wateja wa CRDB benki.

Wengine pichani ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (wapili kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo. Benki ya CRDB imeianza wiki hiyo kwa kuwashukuru wateja wake kwa maoni na ushauri ambao umeiwezesha benki hiyo kutoa huduma bora na zenye viwango vya kimataifa kwa jamii.

Wakati makampuni na taasisi dunia nzima zikiadhimisha ‘Wiki ya Huduma kwa Wateja’ mwaka 2022, Benki ya CRDB imeianza wiki hiyo kwa kuwashukuru wateja wake kwa maoni na ushauri ambao umeiwezesha benki hiyo kutoa huduma bora na zenye viwango vya kimataifa kwa jamii.

Salamu hizo za shukrani zimetolewa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo wakati wa hafla iliyofanyika katika tawi la Benki hiyo lililopo Oysterbay, Jijini Dar es Salaam. Nshekanabo alisema wateja wamekuwa msingi mkubwa kwa Benki ya CRDB kufikia mafanikio ambayo imekuwa ikiyapata kufikia kuwa ‘Benki Bora zaidi Tanzania’.