Jumatatu , 5th Dec , 2022

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Lawrence Mafuru amewataka wanamipango kutekeleza mipango inayoonekana na yenye mafanikio Ili kuweza kufanikisha dira ya mendeleo ya miaka mitano ijayo itakayowezesha mabadailiko ya kiuchumi,na kijamii Kwa kizazi kijacho.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Lawrence Mafuru

Mafuru ametoa Kauli hiyo wakati akizungumza na maafisa mipango,watakwimu,wanademographia kutoka taasisi mbalimbali za wizara ya fedha na mipango ambao wanahusika katika uaandaji ,utekelezaji na na kutoa tathimini ya mipango mbalimbali.

Amesema ni muhimu kuwa na mabadailiko ya kijamii na kiuchumi kwa kizazi kijacho hivyo wanapopanga wawe na mipango yenye uhalisia itakayolenga kutatua changamoto mbalimbali za wananchi hususani kizazi kijacho.

“Nataka kuona kada ya mipango ni muhimu Sana katika mustakabali wa taifa hivyo Ili kuiwezesha tasnia hiyo kutoa mchango stahiki wanamipango ni budi kuwa na taarifa zote zinazotokea nje ya nchi Ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katikà utekelezaji wa mipango yao”.alisema Lawrence Mafuru

Kwa upande wake kamishina wa idara ya mipango ya kitaifa wizara ya fedha na mipango Dokta Musali Milanzi amesema kongamano hilo litawajengea uwezo wanamipango kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mabadailiko ya idadi ya Watu Ili kuweza kuleta mabadailiko ya kiuchumi,kijamii.

Hata hivyo Mafuru amebainisha kuwa nchi Iko katika hatua ya mwisho ya utekelezaji wa dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2020_2023 na tayari maandaizi ya dira mpya ya maendeleo yameanza Ili kutoa mwelekeo mpya wa nchi Kwa miaka 25 ijayo.