Jumatano , 21st Sep , 2022

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Jestas Nyamanga, amewataka Watanzania kuchangamkia fursa ya soko kubwa la Parachichi aina ya hasi yenye viupeleupele kwa kuwa thamani yake ni kubwa na linauzwa kati ya zaidi ya shilingi elfu 10 nchini humo.

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Jestas Nyamanga

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 21, 2022, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao kuhusu fursa mbalimbali kwa Watanzania zilizopo nchini Ubelgiji.

"Tanzania ni ya tatu Ulaya kwa kuuza Parachichi lakini sehemu kubwa ya parachichi letu tunauza kupitia Kenya na tumezungumza na TAHA kuona namna gani tukauza moja kwa moja huku, Parachichi lenye vipelepele lina soko kubwa sana hapa Ulaya," amesema Balozi Jestas

Aidha Balozi ameongeza kuwa, "Parachichi moja inauzwa Euro 4 zaidi ya elfu 10 za Tanzania wakati nyumbani utalinunua kwa shilingi 500 au 1000 sasa ukiuza huku unaweza ukapata faida kubwa mno,".