Jumanne , 4th Oct , 2022

Vijiji kumi na mbili katika halmashauri ya Mtwara vinatarajiwa kupitishiwa bomba la gesi asilia la lenye urefu wa kilomita 35.

Mradi wa gesi asilia

Wananchi na wakazi wa vijiji hivyo wametakiwa kutoa ushirikiano kwa shirika la  maendeleo ya petroli  Tanzania ( TPDC) kwa ajili ya kufanya tathimini  ya mali, na  kulipwa fidia zao, kwa ajili ya kuanza utekelezaji  mradi huo.

Akizungumza  na wananchi wa Kijiji cha  Moma  kata ya Moma  wakati wa kutambulisha mradi huo, Mkuu wilaya ya  hiyo, Dustan Kyobya  amewataka wananchi kupokea mradi huo,  huku Emmanuel Simon meneja  gesi asilia  toka shirika la maendeleo ya petroli Tanzania,  akieleza namna ambavyo matumizi ya gesi asili yameongezeka kutokana na kuwapo kwa ukame hapa nchini.

Baadhi ya wananchi wakazungumzia uwapo wa mradi huo katika vijiji vyao, wamesema ni mradi muhimu na kwamba serikali na wawekezaji wajitahidi kuhakikisha vijiji vinavyopitiwa na mradi huo vinawanufaisha wakazi wa maeneo hayo kwa kutoa fursa za kujiingizia kipato kwa wenyeji.