Viwanda vipya 16 kujengwa kwaajili ya vifaa tiba

Alhamisi , 30th Jul , 2020

Nchi ya Tanzania katika kuhakikisha inatimiza azma ya kuwa nchi ya viwanda na kujitosheleza kwa bidhaa ndani ya nchi imedhamiria kuwekeza kwenye uzalishaji wa ndani.

Adam Fimbo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),

Nchi ya Tanzania katika kuhakikisha inatimiza azma ya kuwa nchi ya viwanda na kujitosheleza kwa bidhaa ndani ya nchi imedhamiria kuwekeza kwenye uzalishaji wa ndani.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo wakati akielezea mafanikio ya serikali y awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli na kuwa miongoni mwa mafanikio ni pamoja na kuanzisha viwanda vya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Fimbo amesema muda mfupi Tanzania itakuwa na viwanda visivyopungua 30 baada ya wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba.

Amesema hadi sasa vipo viwanda 14 na viwanda 16 vipo katika hatua za mwisho kukamilika ujenzi ili kuanza uzalishaji huku wawekezaji wa ndani wakipata mwamko mkubwa katika kuziba ombwe la uagizaji dawa.

"Miaka imesogea na uwekezaji katika sekta ya afya umekua. Naamini utafiti ukifanyika sasa hali itakuwa tofauti na hivyo. Hadi sasa tuna viwanda 14 na viwanda 16 vipo katika hatua za mwisho kukamilika ujenzi ili kuanza uzalishaji. Utaona hii asilimia ya uagizaji itashuka," alisema Fimbo.