Jumatatu , 17th Aug , 2020

Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania imesema kuwa licha ya serikali kuweka mkakati wa kuwainua wakulima kwa kuweka bei elekezi ya mbolea bado changamoto kubwa ipo kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua baadhi ya mbolea zinazozalishwa viwandani (Picha na maktaba)

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dkt. Stephan Ngailo katika mahojiano na EATV ambapo amesema asilimia 90 ya  mbolea inayotumika nchini inazalishwa nje ya nchi huku asilimia 10 pekee ikibaki kwa viwanda vya ndani.
“ Rais wetu Magufuli ameboresha eneo la siasa ya uwekezaji upungufu huo wa mbolea bado sio kikwazo kwa wakulima kulima kilimo chenye tija”

Dkt. Ngailo amesema maandalizi ya usambazaji mbolea kwa wakulima yameanza huku akisisitiza wawekezaji nchini kuchangamkia fursa ya mapinduzi ya viwanda kwa kufungua viwanda vingi vya uchakataji wa mbolea kutokana na mahitaji yake kuongezeka.
“Bado tuna njia ndefu ya kuhamasisha uwekezaji haswa kwenye viwanda vya uzalishaji wa mbolea, mazingira ya uwekezaji yapo wazi ni wafanyabiashara au wawekezaji kuchangamkia fursa hiyo”