
Sheikh mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakari Zubeir
Shekhe mkuu ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa ujumbe wa Mufti kuelekea uchaguzi mkuu.
“Tusitumike na watu wengine kuivuruga amani yetu ambayo mwenyezi mungu ametupatia hii ni tunu ya watanzania wote bila ya kujali dini zao na makabila yao” amesema Mufti
Aidha amewasisitiza watanzania kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kwenda kumchagua kiongozi wanaemtaka