Jumatatu , 27th Feb , 2023

Kuna hofu kwamba zaidi ya watu 100, wakiwemo watoto, wamepoteza maisha  baada ya boti yao kuzama katika eneo baya la bahari kusini mwa Italia. Takriban wahamiaji 62 wamethibitishwa kufariki. 

Meli hiyo ambayo inadaiwa kuwa ilikuwa imebeba watu 200, ilivunjika wakati ikijaribu kutua  siku ya Jumapili. Watu kutoka Afghanistan, Pakistan, Somalia na Iran walikuwa ndani ya boti hiyo.

Miili iliopolewa kutoka ufukweni katika eneo la mapumziko la karibu la bahari katika mkoa wa Calabria, ambapo Kulikuwa na watoto 12 miongoni mwa waathiriwa, akiwemo mtoto mchanga.

Walinzi wa pwani walisema watu 80 wamepatikana wakiwa hai, akiwemo baadhi waliofanikiwa kufika ufukweni baada ya kuzama ikimaanisha wengine wengi bado hawajulikani waliko.

Wengi wa wale waliokuwa ndani ya ndege hiyo walidhaniwa kutoka Pakistan. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Shehbaz Sharif ametaka kufanyika kwa uchunguzi mara moja.