Jumanne , 7th Oct , 2025

Watu wawili akiwemo mwanamke mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 47 wamefariki dunia kwa kuzama mtoni katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wilaya ya Mwanga na Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

Watu wawili akiwemo mwanamke mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 47 wamefariki dunia kwa kuzama mtoni katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wilaya ya Mwanga na Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

Kaimu Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoani Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi, Jeremiah Mkomangi, amesema tukio la kwanza limetokea jana tarehe 6 Mtaa wa Msasani A Kata ya Kaloleni Manispaa ya Moshi likimhusisha mwanamke anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 47 aliyekuwa akitokea shambani, ambaye majira ya saa kumi na moja jioni wakati akipita pembezoni mwa mto Mamba aliteleza na na kuzama katika mto huo.

Baada ya kupokea taarifa hizo jeshi la polisi lilianza juhudi za kumtafuta katika eneo la tukio ambapo alipatikana baadaye akiwa tayari ameshafariki.

Tukio la pili likitokea Mto Kifaru wilaya ya Mwanga, mkoani humo likihusisha mtu aliyekuwa anavuka mto huo kusombwa na maji pia na licha ya kutafutwa toka jana, amepatikana leo majira ya saa nane mchana na mwili wake kukabidhiwa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya taratibu nyingine za kiuchunguzi.

Aidha, Kamanda Mkomangi ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuchukua tahadhari za kiusalama wakati wa kuvuka katika mito hiyo.