
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava amethibitisha vifo vya watu watatu na majeruhi sita kufuatia ajali ya gari aina ya Noah walilokuwa wakisafiria kutokea harusini mkoani Tanga.
DC Mnzava amesema ajali iyo imetokea leo Jumapili Septemba 28, 2025 katika eneo la Njiapanda, wilayani hapa baada ya gari lao aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Korogwe mkoani Tanga, kugongana uso kwa uso na lori lenye tela lililokuwa linatokea Arusha kuelekea Tanga.
Waliofariki dunia wametajwa kuwa ni Samwel Nyerembe (44) mkazi wa Bonite ambaye alikuwa dereva wa Noah, Rebeka Tarimo (29) mkazi wa Soweto na Farida Mazimu (40) mkazi wa Bonite.
Aidha, Majeruhi wametambulika kuwa ni Asia Lyimo (36) mkazi wa Bonite, Zainab Lyimo(38), Mariam Lyimo (39), Salome Oisso (36), Narahat Emmanuel mtoto wa miezi saba na Maira Lyimo mtoto, wote walikuwa kwenye Noah.