
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Wilbroad Mutafungwa, amesema katika oparesheni waliyoifanya kwa siku za hivi karibuni, wamefakiwa kuwakamata watuhimiwa hao huku akitoa wito kwa wamiliki wa Viwanda pamoja na Makampuni binafsi mkoani hapo, kushirikiana na Jeshi hilo kwa lengo la kutatua ufumbuzi wa changamoto za kiusalama.
"Watu wanne kati yao walikamatwa kwenye Bwawa lile wakiwa wanafanya Uvuvi haramu, tumefanikiwa pia kukamata Makasia 4, Mitumbwi 9 pamoja na Nyavu 6" amesema Kamanda Mutafungwa.
Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na kwamba upelelezi utakapo kamilika, watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.