Jumatano , 6th Mei , 2015

Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu 37 kwa kosa la kufanya fujo kwa kuzuia watu wengine kutoa huduma ya usafiri kama bajaji na magari ya watu binafsi kwa kuwapiga watu wanaopanda vyombo hivyo vya usafiri.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma ACP David Misime.

Watu hao wamekamatwa kwenye mitaa ya Nkuhungu katika barabara ya kwenda Singida na Chadulu kwenye barabara ya Morogoro katika manispaa ya Dodoma.

Akifafanua kuhusu kukamatwa kwa watu hao 37 Kamanda wa jeshi la molisi mkoa wa Dodoma ACP David Misime amesema ni wale tu waliokwenda mbali zaidi na kujichukulia sheria mikononi, ila kwa wale wote walioegesha magari yao kwenye vituo au pembezoni mwa barabara hawakukamatwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime ametoa wito kwa watu wote kwamba ni marufuku watu kuzuia wengine kutoa huduma, ni marufuku watu kuharibu mali za wengine.

Na kuongeza kuwa Wanaofanya uhalifu huo watakamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.