Jumatatu , 1st Sep , 2025

Obeida alikuwa miongoni mwa wanachama wachache waandamizi waliosalia wa tawi la kijeshi la Hamas kabla ya shambulio lake baya la tarehe 7 Oktoba 2023 kusini mwa Israel.

Abu Obeida, msemaji wa kundi la wapiganaji la Hamas anayeaminika kuwa na umri wa miaka 40, ameuawa katika shambulio la anga katika mji wa Gaza, Israel imesema.

Hata hivyi bado Hamas haijathibitisha kifo chake. Kundi hilo la wapiganaji wa Palestina hapo awali lilisema makumi ya raia waliuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye jengo la makazi katika weneo hilo.

Waandishi wa habari katika eneo hilo wameripoti kuwa takriban watu saba wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mashambulizi hayo katika kitongoji chenye wakazi wengi cha al-Rimal katika mji wa Gaza, huku watoto wakiwa ni miongoni mwa waliojeruhiwa.

Katika chapisho lake kwenye mtandao wa X zamani Twitter, Katz, Waziri wa Ulinzi wa Israel amelipongeza jeshi la Ulinzi la Israel( IDF) na wakala wa Israel, Shin Bet kwa kazi hiyo baada ya jana Jumapili kuonya kwamba wengi zaidi wa washirika wa uhalifu wa Obeida wangelengwa na kuongezeka kwa kampeni huko Gaza, rejeleo la mpango ulioidhinishwa hivi karibuni wa Israeli wa kutwaa udhibiti wa Jiji la Gaza kwa ujumla.

Obeida alikuwa miongoni mwa wanachama wachache waandamizi waliosalia wa tawi la kijeshi la Hamas kabla ya shambulio lake baya la tarehe 7 Oktoba 2023 kusini mwa Israel.

Makombora matano yalipiga ghorofa ya pili na ya tatu katika jengo la ghorofa sita katika kitongoji cha al-Rimal kwa wakati mmoja kutoka pande mbili tofauti.

Katika kile ambacho kinaweza kuwa hotuba yake ya mwisho siku ya Ijumaa, Obeida alisema hatma ya kubaki mateka wa Israel itakuwa sawa na ile ya wapiganaji wa Hamas, akiionya Israel dhidi ya mpango wake wa uvamizi katika mji wa Gaza.