
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Temeke Dar es Salaam Mh. Ngeka amemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini Tshs 300,000/= mshtakiwa Adela Ndela Zakaria mwenye umri wa miaka 25, Mkazi wa Viwawa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kutupa mtoto jalalani mwanzoni mwa mwezi Septemba 2025.
Imeelezwa kuwa Mshtakiwa mwezi Aprili 2025 alitoka Mbeya kwa ajili ya kuja Dar es Salaam kufanya kazi za ndani, baada ya kupokelewa na mwenyeji wake anayeishi Keko Dar es Salaam alimchukua nyumbani kwake ili asubirie kuanza kazi kumbe alikuwa mjamzito na alificha ndipo asubuhi majirani waliona kichanga jalalani na baada ya kufuatilia aligundulika huyo mwanamke ndio aliyefanya hivyo na alipohojiwa alikiri kwamba alizaa mtoto wa kike na kisha alimuacha jalalani ili asigundulike kama amezaa na aweze kwenda kufanya kazi.