Makonda ameyazungumza hayo alipokuwa akihutubia kwneye sherehe za uzinduzi wa foundation na manukato ya msemaji wa Simba Haji Manara, na kueleza kwamba bara la Afrika tuna laana na chuki binafsi, ndio maana watu wengi hawaendelei, lakini kwa mjini kitu ambacho kinasababisha watu waendelee kuwa masikini ni majungu na fitina.
“Hata mtoto akifanya vizuri darasani anapigwa tu jini, unashangaa tu mtoto anarudi nyumbani hawezi kuona, mtihanmi ukija haelewi, sisi ndio tunaongoza kwa kurogana mwenyewe mtu asifanikiwe, uchawi wa mjini ni majungu, fitina chuki”, amesema Makonda.
“Afrika kwa miaka mingi ina laana ya umasikini, na laana hii imepokelewa kwa muda mrefu, na sisi tumekuwa mashuhuda na wabeba maono ya laana, ukitaka kujua kama una laana ni pale unaponuna mwenzako anapoanza kufawakifanikiwa".
"Hii ndio laana inayotutesa sisi, na ndio maana waliokuwa wamekulia vjijini kama sisi, mtoto atakayekuja nyumbani kutoka mjini akaanza kujenga nyumba ya tofali na kuweka bati lazima afe, inafika kipindi mtoto anaogopa kurudi kijijini kwao kwa sababu anafahamu, wachawi walikuwa wanajulikana”, amesema Makonda.





.jpg?itok=5cvL0YaP)