
Amesema licha ya baadhi ya wadau kubadilisha sera na mwelekeo wa usaidizi wao, Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka afya ya Watanzania kuwa kipaumbele, huku juhudi dhidi ya UKIMWI zikiimarishwa zaidi.
Rais Samia pia amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu, huduma za tiba na kinga kwa wote ili kufikia malengo tuliojiwekea