Ijumaa , 28th Nov , 2025

Wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, Mjumbe wa Kamati kuu, Rose Mayemba na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia.

Maombi namba 25480/2025 yaliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Zanzibar, Saidi Issa na wenzake wawili dhidi ya viongozi wa chama hicho ya kukiuka amri ya Mahakama ya kutofanya siasa inatarajiwa kuendelea kusikilizwa leo Ijumaa, Novemba 28 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam.

Wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, Mjumbe wa Kamati kuu, Rose Mayemba na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia.

Washtakiwa wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Habari, Gerva Benard Lyenda, Hilda Newton, Twaha Mwaipaya na Bodi ya wadhamini wa chama hicho.

Wakati Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo, Chadema katika taarifa iliyoitoa jana Novemba 27, 2025, imewataka wanachama wake kufika mahakamani hapo ili kusikiliza uamuzi wa kesi hiyo.