Alhamisi , 3rd Nov , 2016

Serikali imesema kuwa imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuwapangia maeneo ya biashara wafanya bishara wadogo (Machinga) ili kuwaondoa katika maeneo yasiyostahili ikiwemo barabarani.

Naibu Waziri TAMISEMI, Selemani Jafo

 

Akijibu swali la mbunge wa Mtwara Mjini Maftah Nachuma aliyehoji sababu za wamachinga kuondolewa katikati ya mji kinyume na agizo la Rais, Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo amesema kuwa agizo la Rais halikumaanisha wamachinga waachwe barabarani, bali aliagiza watafutiwe maeneo yenye biashara jambo ambalo tayari limetekelezwa katika miji mbalimbali ikiwemo Mtwara.

Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene amekiri kuwa tatizo la wamachinga siyo maeneo bali maeneo yenye biashara, hivyo kuziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo ambayo yatakuwa yanafikiwa kirahisi na wateja kabla ya kuwahamisha.

Kufuatia tatizo hilo kujirudia, Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula ameishauri wizara hiyo kuziongozea fedha halmashauri ili ziwe na nguvu ya kifedha ya kutayarisha maeneo yenye biashara nzuri kwa wamachinga.

Sikiliza hapa hali ilivyokuwa leo bungeni

Ufafanuzi kuhusu maagizo ya Rais juu ya machinga kutobugudhiwa.
Joseph Mbilinyi Vs Naibu Spika